1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mtu mmoja auawa, zaidi ya 200 wajeruhiwa maandamano ya Kenya

21 Juni 2024

Mtu mmoja ameuawa, 200 wamejeruhiwa na wengine zaidi ya 100 wamekamatwa kote nchini Kenya, wakati polisi walipozima maandamano ya kitaifa dhidi ya mipango ya serikali ya kuongeza kodi.

https://p.dw.com/p/4hLkc
Kenya | maandamano Nairobi
Muandamanaji akitumia mwamvuli kujikinga na maji ya kuwashwa kutoka magari ya polisi jijini Nairobi, Kenya, siku ya Jumatano (20 Juni 2024).Picha: LUIS TATO/AFP/Getty Images

Rex Kanyike Masai alifariki jijini Nairobi kutokana na kile kinachoaminika kuwa jeraha la risasi usiku wa Jumatano (Juni 20). Polisi ya Kenya ilisema ingelifanya uchunguzi wa kifo hicho.

Muungano wa mashirika ya kutetea haki za binaudamu umesema serikali ya Rais William Ruto inalenga kukusanya dola bilioni 2.7 kupitia kodi za ziada. 

Soma zaidi: Wakenya waandamana kupinga ongezeko la kodi

Waandamanaji wanaitaka serikali kuachana kabisa na mswada huo, wakisema utaudidimiza uchumi na kuzidisha ugumu wa maisha kwa Wakenya.

Lakini Shirika la Fedha Duniani (IMF) linasema serikali ya Kenya inahitaji kuongeza mapato yake ili kupunguza nakisi ya bajeti na viwango vya ukopaji.