1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaUlaya

Ajificha kwenye matairi ya ndege kutoka Algeria-Ufaransa

29 Desemba 2023

Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 20, amekutwa akiwa hai baada ya kujificha kwenye sehemu ya matairi ya ndege iliyosafiri kutoka Algeria hadi Ufaransa.

https://p.dw.com/p/4ahAi
Paris | Magari ya uwokoaji na wagonjwa yakiwa yameegeshwa nje ya uwanja wa ndege wa Paris Ufaransa.
Mgari ya uwokoaji na gari la wagonjwa yakiwa yameegeshwa mbele ya uwanja wa ndege wa Paris nchini Ufaransa.Picha: Christophe Ena/AP Photo/picture alliance

Kijana huyo aligunduliwa na wakaguzi wa ndege akiwa katika hali mbaya kiafya na baadaye aliwahishwa hospitalini.

Ndege hiyo ya abiria ilitokea mji wa Oran na kutua jana katika uwanja wa ndege wa Orly mjini Paris. Kulingana na takwimu ya mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Marekani (FAA), watu 132 walijaribu kusafiri kwa kutumia mfumo huo kati ya mwaka 1947 na 2001.

Soma pia:UN: Mamia ya wahamiaji wamekufa robo ya kwanza ya 2023

Kwa kawaida, ndege hizo za abiria hupaa angani hadi kwa urefu wa futi 30,000 hadi 40,000 ambapo nyuzijoto hushuka mno hadi kufikia karibu chini ya 50 kipimo cha Celsius na hivyo kuwa hatari kwa mtu anayesafiri katika eneo la matairikukosa hewa na kukabiliwa na baridi kali.