Poland yakataa kucheza na Urusi mechi ya Kombe la Dunia
27 Februari 2022Mpinzani mwingine anayetarajiwa kucheza na Urusi, Sweden, pia wameunga mkono hatua hiyo.
"Hatuwezi kujifanya kuwa hakuna kinachoendelea," alichapisha Robert Lewandowski kwenye ukurasa wake wa Twitter.
soma UEFA kuivua Moscow uenyeji wa fainali ya Ligi ya Mabingwa
Nyota wa Bayern Munich Robert Lewandowski alikuwa mmoja wa wachezaji wengi wa Poland waliounga mkono mara moja uamuzi wa Chama cha Soka Poland kugomea mechi ijayo ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Urusi.
Haya ni maandamano ya hivi punde kutoka kwa ulimwengu wa kandanda dhidi ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, huku vilabu vikiwa vimesitisha udhamini na makampuni ya Urusi. Awali shirikisho la kandanda UEFA waliipokonya Urusi uwenyeji wa fainali ya ligi ya Mabingwa kutoka uga wa Saint Petersburg.
Kufikia sasa, hata hivyo, hakujakuwa na hatua kutoka kwa waangalizi wa kimataifa FIFA kupiga marufuku Urusi kushiriki katika Kombe la Dunia, au hata UEFA kuvifukuza vilabu vya Urusi kutoka kwa mashindano yake.
Chama cha soka cha Poland wamechukulia hatua suala hilo mikononi mwao, huku rais wa shirikisho hilo Cezary Kulesza akiandika kwenye Twitter, "Hakuna maneno zaidi , ni muda wa vitendo!,"
soma FIFA kuzungumza na wadau wa soka juu ya Kombe la Dunia
Mataifa hayo mawili yalitarajiwa kumenyana mjini Moscow mwezi ujao, huku mshindi akicheza na Sweden au Jamhuri ya Czech kuwania kufuzu kwa Kombe la Dunia huko Qatar.
Sweden baadaye iliunga mkono msimamo wa Poland. "Timu ya kitaifa ya wanaume haitacheza dhidi ya Urusi, bila kujali ni wapi mechi itachezwa," shirikisho la soka la Sweden lilichapisha kwenye Twitter.
Rais wa Poland Andrzej Duda na waziri mkuu Mateusz Morawiecki pia walionyesha kuunga mkono hatua hiyo.
Vilabu vya Bundesliga vinaonyesha mshikamano na Ukraine
Vilabu vya Bundesliga vyote vilikaa kimya kwa dakika moja kabla ya mechi zao Jumamosi, katika kuonyesha mshikamano na watu wa Ukraine kufuatia uvamizi wa Urusi. Pia kulikuwa na ishara kama hizo katika ligi zingine.
Ishara ndogo za mshikamano zilionyeshwa ndani na nje ya viwanjani wakati wa mechi za kandanda za Ujerumani siku ya Jumamosi, huku mashabiki na vilabu mbalimbali. Kulikuwa na bendera za Ukraine zilizotawanyika katika viwanja vya Bundesliga.
Katika mechi kati ya Greuther Fürth na FC Köln mashabiki walibeba mabango yalioandika maneno ya kusema "Sitisha vita, tunapinga vita" wakati wa mechi iliyokamilika kwa sare ya moja moja.
soma Raundi ya mtoano ya 16 bora Champions League kuanza
Mabingwa Bayern Munich wakiwa ugenini mjini Frankfurt, uwanja uliwekwa skirini zilizoonyesha rangi za bendera ya Ukraine na ujumbe wa "Stop it, Putin".
Katika ligi ya Premier League, wachezaji wa Manchester United na Watford, pamoja na kocha wa United, Ralf Rangnick, walipiga picha mbele ya ishara ya amani kabla ya mechi kuanza.
Nchini Italia, mechi zote za Serie A ziliahirishwa kwa dakika tano katika kuashiria mshikamano wa kupinga uvamizi wa Ukraine.
https://p.dw.com/p/47eIt '/ https://p.dw.com/p/47egf