Raila: Sishiriki mdahalo sababu Ruto ni fisadi
25 Julai 2022Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari, sekretariati ya muungano huo imesema Raila hawezi kushiriki kwenye jukwaa moja na mtu ambaye hana maadili ambaye ni mgombea urais wa Kenya Kwanza William Ruto.
Taarifa hiyo iliyotolewa na msemaji wa sekretariati ya chama cha ODMProfesa Makau Mutua imesema, mpinzani mkuu wa Raila, William Ruto katika safari yake ya siasa ameonesha kuwa ni fisadi na kwamba ana tamaa ya uongozi.
Imeongeza kusema kuwa iwapo masuala hayo hayatajadiliwa kwenye mdahalo wa siku ya Jumanne yatakuwa makosa makubwa kwa Wakenya na ndio sababu Raila hatashiriki kwenye jukwaa moja na mtu ambaye hana maadili ya msingi.
Mutua amekosoa kikundi cha Ruto kwa kujaribu kufumbia macho masuala ya ufisadi, uadilifu na uongozi ambayo ni makuu kwa wakenya.
Soma zaidi:Kampeni za uchaguzi Kenya zashika kasi
Esther Pasaris ni mwakilishi wa wanawake wa Nairobi kwa chama cha ODM, ameonesha kuunga mkono msimamo wa Odinga kwa hoja kwamba ni bora maswali ya wapiga kura kuliko mpinzani wake wa kisiasia Ruto.
"Naunagana na Raila Odinga anaposema heri niende kuulizwa maswali na wanachi, badala ya kuelekea kwenye mjadala huo na kufanya kichekesho" Alisema Pasaris.
Aliongeza kwamba wanazo taarifa za mbinu chafu za propagandazinazofanywa na upande wa pili ambao ni mpinzani wa karibu wa Odinga Ruto akitaja kwa jina la tangatanga kuwa ni za hali ya juu.
Katika kuweka ratiba yake sawa kwenye kusaka kura za wakenya Raila ameamua kuwa na mazungumzo na wapiga kura siku hiyo ya mjadala ambapo Wakenya watapewa nafasi ya kuelezea suluhisho kwa changamoto zinawakabili.
Ruto:Odinga hana ajenda muhimu kwa wakenya
Hata hivyo Ruto ameitaja hatua ya Raila ya kutohudhuria mdahalo huo ambao umeonekana kufuatiliwa na wadau mbalimbali wa uchaguzi kuwa ni ishara ya kushindwa kwenye uchaguzi mkuu.
wakati yeye mwenyewe akijiweka mguu sawa katika mdahalo huo na kuandaa kile alicghokiita ni ajenda kwa wakenya Ruto amesema mpinzani wake wa karibu Odinga ambae amewahi kugombea nafasi ya Urais mara kadhaa kuwa hana ajenda ya kuwasilisha kwa wakenya katika mdahalo huo utaofanyika wiki hii.
Soma zaidi:Tume ya IEBC yaandamwa kuhusu karatasi za kupigia kura
Katika hatua nyingine idara ya Upelelezi wa Jinai sasa imesema kuwa raia wa Venezuela waliokamatwa siku ya Alhamisi wakiwa na vibandiko vya Uchaguzi sio wafanyikazi wa kampuni ya Kimataifa ya Smartmatic, iliyopewa zabuni na Tume ya Uchaguzi ya IEBC kusafirisha mitambo ya teknolojia itakayotumika kwenye uchaguzi mkuu.
Ripoti zinasema kuwa raia hao wametimuliwa nchini. Vifaa walivyokamatwa navyo vinashikiliwa kwenye afisi za idara ya Jinai .
Hillary Mutyambai ni Inspekta Mkuu wa Polisi amesema kwamba vibandiko hivyo havikutangazwa kwa mujibu wa sheria pili maafisa wa IEBC hawakuwepo vibandiko hivyo .
"Vilipokamatwa kama inavyohitajika, halafu vibandiko hivyo muhimu vilibebwa kwenye begi la mgeni.” Alisema Mutyambai.
Hayo yanajiri huku afisi za Naibu wa Rais William Ruto zilizoko jijini Nairobi zikivamiwa na maafisa wa Uplelezi wa Jinai.
Mratibu Mkuu wa Nairobi James Mugera, amesema kuwa kitendo hicho kililenga kudhibitisha madai ya kuwa sava za uchaguzi zilikuwemo humo. Hata hivyo hazikupatikana.
Zimesalia siku 14 kwa uchaguzi mkuu nchini Kenya kufanyika huku Tume ya Kusimamia Uchaguzi ikiwa na kibarua cha kuonesha umma kuwa itaendesha uchaguzi huru na wa haki.