Rais wa Moldova akosoa uvamizi dhidi ya uhuru na demokrasia
21 Oktoba 2024Rais Sandu ameitoa kauli hiyo baada ya matokeo ya awali ya uchaguzi wa Jumapili kuonyesha kuwa asilimia 55 ya wananchi wa Moldova walichagua "hapana" katika kura ya maoni iliyotaka kuamua ikiwa Moldova inapaswa kujiunga na Umoja wa Ulaya.
Kauli ya rais Sandu ambaye anaunga mkono taifa lake kujiunga na Umoja wa Ulaya na ambaye anaongoza katika uchaguzi wa rais imetolewa huku kukiwa na hofu ya kwamba Urusi ilingilia na kuvuruga matokeo ya uchaguzi huo.
Soma pia: Raia Moldova wapiga kura kumchagua rais, kuamua hatma ya kujiunga EU
Rais Maia Sandu amewaambia wafuasi wake katika mji mkuu Chisinau, kwamba Moldova imekabiliwa na shambulio ambalo halijawahi kushuhudiwa dhidi ya uhuru na demokrasia ya nchi hiyo na kuongeza kuwa makundi ya wahalifu yamejaribu kudhoofisha mchakato wa kidemokrasia.