1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani: NATO yapaswa kujiimarisha kufuatia vita Ukraine

3 Oktoba 2023

Mkuu wa jeshi la Ujerumani, Jenerali Carsten Breuer, ameonya kuwa vita nchini Ukraine vinaweza kuongezeka huku akitoa wito wa kuimarishwa kwa uwezo wa Ujerumani na Jumuiya ya Kujihami ya NATO.

https://p.dw.com/p/4X4y2
Generalleutnant Carsten Breuer
Picha: Annette Riedl/dpa/picture alliance

Breuer amesema dalili za kabla ya kunyakuliwa kimabavu kwa Rasi ya Crimea mnamo mwaka 2014 na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine  mwaka jana, hazikuzingatiwa kwa wakati muafaka.

Amesema uvamizi huo haramu unasisitiza umuhimu wa kuwepo vikosi vya jeshi vilivyo tayari kwa mapambano.

Hayo yanajiri wakati Urusi imesema hii leo kuwa haijasitisha majaribio yake ya nyuklia, na imekua mara kadhaa ikiyaonya mataifa ya Magharibi kuwa shambulio lolote dhidi yake linaweza kusababisha majibu ya nyuklia.