1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baraza la Haki za Binaadamu la UN lalaani ukandamizaji Iran

25 Mei 2023

Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa limepiga kura jana Alhamisi, kulaani ukandamizaji wa umwagaji damu dhidi ya maandamano ya amani nchini Iran. Hatua hiyo inalenga kushinikiza mabadiliko nchini Iran.

https://p.dw.com/p/4K2rm
Baerbock bei Sondersitzung des Menschrechtsrates
Picha: picture alliance/photothek

Azimio hilo lililotolewa na Ujerumani na Iceland liliungwa mkono na nchi 25 ikiwa ni pamoja na Marekani na nchi nyingi za Ulaya, Amerika Kusini, Asia na Afrika. Nchi sita ambazo ni China, Pakistan, Cuba, Eritrea, Venezuela na Armenia zilipinga hatua hiyo, huku nchi 16 zikijizuia kupiga kura.

Soma pia: UN yaitaka Iran kusitisha kamatakamata ya waandamanaji

Afisa mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Turk, alitoa wito hapo awali kwa serikali ya Iran kusitisha ukandamizaji dhidi ya waandamanaji, lakini Mjumbe wa Tehran katika Baraza hilo amesema kuwa kikao hicho kimechochewa kisiasa.

UN Menschenrechtsrat | Volker Turk
Afisa mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker TurkPicha: Martial Trezzini/KEYSTONE/picture alliance

Maandamano hayo yalichochewa na kifo cha Mahsa Amini, msichana wa Kikurdi mwenye umri wa miaka 22, zaidi ya miezi miwili iliyopita akiwa chini ya ulinzi wa  polisi wa maadili kwa kukiuka sheria kali za mavazi ya Kiislamu nchini Iran.

Ujerumani yasema ni hatua ya ujasiri

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock, ambaye alihudhuria kikao hicho amesema hali hiyo ilikuwa ni jaribio la ujasiri wa Umoja wa Mataifa ambao ulianzishwa ili kulinda uhuru wa kila taifa, lakini utawala unaotumia mamlaka hayo kukiuka haki ya watu wake, basi unakiuka pia maadili ya Umoja wa Mataifa.

Soma pia: Macron atoa wito wa vikwazo vya kimataifa kwa maafisa wa Iran

Baerbock ameendelea kuwa mara kadhaa wamekuwa wakiitaka Iran kuheshimu haki na kukomesha ukatili dhidi ya waandamanaji, umwagaji damu, mauaji ya kiholela, kukamatwa kwa watu wengi, adhabu ya kifo, lakini jibu pekee walilopokea lilikuwa kuongezeka kwa vurugu na vifo zaidi.

Kikao cha kushinikiza mabadiliko

Michele Taylor, Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa amesema dhamira ya kikao hicho ni kushinikiza mabadiliko na kupinga ukandamizaji.

Schweiz Genf | Annalena Baerbock bei Sondersitzung des Menschrechtsrates
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock.Picha: Thomas Koehler/photothek/picture alliance

"Dhamira ya kutafuta ukweli ni muhimu kabisa ili sio tu kukuza uwajibikaji, lakini tunajua kuwa kutokujali kunasababisha ukiukwaji zaidi wa haki za binadamu, na bila utaratibu kama huu, hatuwezi kutarajia mabadiliko yoyote, na mabadiliko lazima yatokee sasa."

Khadijeh Karimi, Mkurugenzi katika Ofisi ya naibu Makamu wa rais wa Iran anayehusika na masuala ya Wanawake na Familia, amezikosoa juhudi za Maitaifa ya Magharibi na kusema hatua hiyo ilichochewa kisiasa na ina lengo la kupotosha hali ya haki za

Karimi amezituhumu pia nchi hizo kwa kufumbia macho ukiukwaji wa haki katika maeneo kama Yemen, Palestina, au dhidi ya jamii za

Kikao cha jana huko Geneva nchini Uswisi, ni juhudi za hivi punde za kimataifa kuweka shinikizo kwa Iran juu ya ukandamizaji wake, ambao tayari umeibua vikwazo vya kimataifa na hatua zingine. Tume hiyo inatarajiwa kutoa ripoti yake kwenye baraza hilo katikati mwa mwaka ujao wa 2023.