1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUturuki

Upinzani Uturuki waungana dhidi ya Erdogan

Daniel Gakuba
7 Machi 2023

Muungano wa vyama sita nchini Uturuki umemteua kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini humo Republican's People's Party - CHP, Kemal Kilicdaroglu, kama mgombea atakayepambana na Rais Recep Tayyip Erdogan.

https://p.dw.com/p/4OL0K
Türkei | Oppositionspartei CHP, Kemal Kilicdaroglu
Picha: Dilara SenkayaREUTERS

Muungano wa vyama sita nchini Uturuki umemteua kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini humo Republican's People's Party - CHP, Kemal Kilicdaroglu, kama mgombea atakayepambana na Rais Recep Tayyip Erdogan katika uchaguzi wa mwezi Mei 14.

Hatua hii imehitimisha miezi ya mifarakano na mivutano iliyokuwa imewavunja moyo wafuasi wa upinzani.

Muafaka huo umefikiwa saa chache baada ya mwanachama muhimu wa muungano huo Meral Aksener, ambaye anakiongoza chama cha kizalendo cha Iyi na ambaye alikuwa anaupinga uteuzi wa Kilicdaroglu, kukubali suluhisho lililowekwa mezani na kurudi katika muungano huo.

Erdogan ambaye amekuwa kwenye kilele cha siasa za Uturuki tangu mwaka 2003, anakabiliwa na upinzani mkubwa katika uchaguzi ujao, ambao wachambuzi wanasema ndio muhimu zaidi nchini humo kwa muda wa karne nzima.