You need to enable JavaScript to run this app.
Nenda kwenye maudhui
Nenda kwenye orodha kuu
Nenda tovuti zaidi za DW
Vidio zetu
Sauti zetu
Maeneo
Tanzania
Kenya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Afrika
Ulaya
Mada
Haki za binadamu
Mazingira
Afya
Teknolojia
Kategoria
Matukio ya Kisiasa
Masuala ya Jamii
Michezo
Yanayoangaziwa
Uchaguzi Mkuu wa Ujerumani 2025
Mzozo wa Israel na Hamas
Bundesliga
Sauti zetu
Vidio zetu
Matangazo
Picha: DW
Vidio zetu
Tazama vidio zetu hapa
Ruka sehemu inayofuata Maudhui yote kwenye mada hii
Maudhui yote kwenye mada hii
Mtetezi wa watoto wenye usonji
Msichana Jasiri: Lembe binti wa Kitanzania wa mfano wa kuigwa katika juhudi ya utetezi wa watoto wenye usonji.
Shambulizi la roketi lauwa watu 12 katika milima ya Golan
Shambulizi lililolenga katika uwanja wa michezo lauwa vijana 12 wakimwemo watoto wadogo wa hadi umri wa miaka 12.
Msichana jasiri aliyejitosa fani ya kuchomelea vyuma
Katika umri wa miaka 19, Sharifa Karim amekuwa msichana hodari na jasiri katika fani ya uchongaji na uchomeleaji vyuma. Anasema haikuwa rahisi wakati alipoanza kutokana na fani hii kuwa na idadi kubwa ya wanaume lakini anaona ufahari kuifanya kazi hii. #msichanajasiri
Monica Mkama Msichana Jasir Mjasiriamali
Monica ni msichana ambaye ameamua kujiajiri akiwa bado ni mwanafunzi, huku akiitumia biashara yake katika kuupiga kumbo umasikini. Kutokana na juhudi zake wapo ambao wamejifunza kutoka kwake. Je ni vipi aliweza kutoka kumiliki biashara moja hadi tatu?
Trump akubali kuwa mgombea wa Republican 2024
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump amekubali rasmi uteuzi wa kuwania urais kwa tiketi ya Chama cha Republican katika mkutano mkuu uliotawaliwa zaidi na jaribio la mauaji dhidi yake.
Kurunzi Ujerumani: Tamasha la kulenga shabaha
Katika miji na vijiji vingi nchini Ujerumani, matamasha ya kulenga shabaha, maarufu kama “Schützenfest” hufanyika mara moja kwa mwaka.
Simba na Yanga zajiimarisha kuelekea msimu mpya wa soka
Kando na Clatous Chama, Yanga imewasijili Khomeini Abubakar na Boka Chadrak. Je, umeridhika na usajili wa klabu yako?
Unajua namna Yoga inavyoweza kukusaidia kiafya?
Nina uhakika unajua kitu kuhusu mazoezi ya Yoga, lakini unajua umuhimu wake kiafya? Kuna mengi unayoweza kujifunza ama kumshirikisha mwenzako kuhusu mazoezi haya. Tizama video hii kujifunza zaidi. #Kurunzi
Kituo cha elimu ya awali kwa watoto wakimbizi
Jamii za wakimbizi na wenyeji Kaskazini Magharibi mwa Uganda wameanzisha vituo vya kutoa elimu ya awali kwa watoto. Walimu na walezi ni wanajamii ambao wamejitolea kuendesha shughuli hiyo baada ya kupokea mafunzo maalum. Ebu tazama vidio na uwapongeze walimu hawa.
Dalili za tatizo la PCOS kwa wanawake
Wanawake wengi wenye ndevu ama nywele za usoni wanakabiliwa na matatizo ya kiafya ya PCOS yanayohusiana na homoni. Dalili nyingine za PCOS ni kuongezeka uzito, uso wenye mafuta na ugumu wa kubeba ujauzito. #kurunziafya #wanawake #pcos #afya
Neema Athuman: Muigizaji mdogo wa Tanzania
Neema Athuman: Muigizaji mdogo wa Tanzania
Monica Pereira ni DJ na mwalimu kutoka Cape Verde
Monica Pereira amevutia hisia za watu wa Cape Verde kwa kuwa maarufu kama DJ na mwalimu. Mapenzi yake ya muziki na hitaji la kupata pesa ndio sababu zilizomfanya aingie kwenye vilabu vya usiku, eneo ambalo bado linatawaliwa na wanaume nchini humo. Ebu tazama vidio na umpe neno mpambanaji huyu.
Fahamu namna ambavyo mionzi dawa inavyotengenezwa Tanzania
Cyclotron Kiube ni aina Mionzi dawa ambayo hutumika katika uchunguzi wa awali wa saratani kwa kupiga picha kwa kutumia PET-CT Scan ili kujua hatua ya saratani na kumsadia mtaalamu kujua ni aina gani ya dawa ambayo itakua na msaada kwa mgonjwa.
Germany inakabiliana vipi na uhalifu wa ukoloni Tanzania?
Ujerumani bado inaendeleza juhudi zake za kujivua gamba na yaliyotokea katika kipindi cha ukoloni nchini Tanganyika ambayo ni Tanzania bara ya sasa, mafuvu kadhaa ya binadamu walionyongwa yalisafirishwa kutoka nchini humo hadi Ujerumni kuhifadhiwa. Sasa familia za wahusika wameweka madai mezani. Sikiliza mahojiano.
Kituo cha kuwalea watoto bila malipo Nairobi
Huwa ni changamoto kubwa kwa mzazi aliye na mtoto mdogo kwenda kuchakarika kutafuta riziki. Lakini kuna mama mmoja Nairobi aliyeanzisha kituo kinachotoa suluhisho: kuwalea watoto saa za mchana bila malipo.
Matumizi yaliokithiri ya muguka na madhara yake kiafya
Matumizi mabaya ya muguka na dawa zingine za kulevya yamesababisha ongezeko kubwa la waraibu katika vituo vya kurekebishia tabia. Hata hivyo viongozi wa Mombasa kupiga marufuku usafirishwaji na uuzwaji wa aina hiyo ya bidhaa. Tazama video kuona madhara yake kiafya.
Hedhi salama bado ni changamoto kwa wasichana
Hapo kabla ilikua ni nadra kulizungumzia suala la hedhi hadharani lakini muda inavyozidi mambo kuwekwa wazi hili linawapa nafasi wasicha kuzungumza suala hili kwa uwazi zaidi. #MsichanaJasiri
Matumizi ya AI kwa lishe bora
Ndoto ya Janet Kitsovi ni kuona ubunifu wake wa akili mnemba Plate-AI na matumizi yake yanawasaidia wagonjwa wengi wanaougua kisukari, moyo na shinikizo la damu nchini Tanzania, Afrika na kwingineko ulimwenguni.
Kurunzi Live Hedhi Salama Day
Wakati ulimwengu ukiadhimisha siku ya Hedhi Salama, bado wasichana na wanawake wengi wanakabiliwa na changamoto mbalimbali wanapofikia kwenye siku hizo. Je kipi kifanyike kuwasaidia? Tizama video hii kisha utuambie.
Filamu ya Kitanzania "Kaburi wazi" yazua mjadala Köln
Athari za ukoloni bado zinashuhudiwa katika mataifa mengi barani Afrika, lakini katika kipindi cha takriban karne moja ya ukoloni wa Ujerumani nchini Tanganyika ambayo ni Tanzania bara ya sasa, Je, Wajerumani wanatilia maanani kile babu zao walikitenda katika taifa hilo la Afrika mashariki? Tazama mjadala na majibu katika filamu ya "Kaburi wazi".
Wasichana wa sasa katika kuzienzi tamaduni zao
Katika safu yetu ya Msichana Jasiri, mjadala unaopewa nafasi unahusu. "Wasichana katika kuzienzi tamaduni zao."
Mafuriko yaacha homa ya mapafu kwa watoto Kenya
Mvua kubwa zilizoambatana na mafuriko zimeacha athari za kiafya kwa watoto wengi katika maeneo ya mabanda nchini Kenya
Msomi wa uchumi na mbunifu wa mapambo ya ndani ya kitamaduni
Kutoka kuwa mwanauchumi mpaka kutumia stadi za mikono katika kujiajiri hii haikuwa rahisi kwake, lakini ule msemo waelimu ni ufunguo wa maisha kwake anautendea haki anaitumia elimu yake ili kuhakikisha kuwa anapata bidhaa zenye ubora na hata kuzitangaza kwa kutumia majukwaa mbalimbali huku akiwa na matarajio ya kufika katika soko la kimataifa.
Wasichana na wanawake wanavyotumia fursa ya teknolojia
Kuwekeza katika elimu ya teknolojia ya akili ya kubuni (AI) kwa wasichana sio tu kunafungua uwezo wao bali pia huchochea uvumbuzi na utofauti katika tasnia ya teknolojia kwa baadae. Taasisi ya LP digital kutoka Tanzania inafanya jukumu hilo la kutoa mwanga wa sayansi bunifu kwa wasichana.
Kutibu majeraha yaliosababishwa na vita Ukraine
Zaidi ya wanajeshi elfu ishirini waliojeruhiwa walifika katika hospitali ya Mechnikov katika eneo la Dnipro, tangu Urusi ilipoivamilia kikamilifu Ukraine mnamo Februari 2022. Daktari Valentyna Lisnycha katika hospitali hiyo inayotibu wanajeshi waliojeruhiwa vitani pamoja na timu yake wamejitolea kuokoa maisha ya askari.
Kurunzi Live: Maoni ya Wananchi juu ya Muungano
Wakati Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ukikaribia kutimiza miaka 60, Watanzania wamekuwa na maoni tofauti kuhusiana na muungano huo. Je wanahisi kama bado una umuhimu kwao ama la? Tizama video hii kwa mengi zaidi, kisha utupe maoni yako.
Wanawake wenye ulemavu wajiunga na mchezo wa mpira wa mikono
Kutana na wanawake hawa wenye ulemavu waliamua kujiingiza kwenye mchezo wa mpira wa mikono na namna wanavyosakata mchezo huo.
Mwanaharakati wa haki za watoto wa mitaani Tanzania
Kundi la watoto wa mtaani ni kundi ambalo linaendelea kuongezeka kwa kasi huku watoto hawa wakiwa hawana elimu madhubuti kutokana na ukatili wanaokutana nao, lakini juhudi za wanaharakati wa masuala ya kijamii ni zipi katika kuhakikisha kuwa wanalisaidia kundi hili. Jackline Joseph ni mwanaharakati ambaye amejitolea katika kulisaidia watoto katika kuwapatia elimu dhidi ya ukatili.
Chipukizi wa muziki wa kizazi kipya
Precious ni mwanamuziki chipukizi wa kizazi kipya kutoka Tanzania ambaye Uwezo wake wa kutumbuiza katika majukwaa umempa sababu ya kuwa mfano kwa watoto wengine. Anasema baba yake ndiye aliyempa msukumo mkubwa wa kunoa kipaji chake. #msichanajasiri.
Umewahi kuombwa ama kutoa rushwa?
Rushwa ni tatizo la Kidunia lenye madhara makubwa kwa mtu, jamii, hadi ngazi ya taifa. Rushwa imetumiwa kupoka haki stahili kwa watu na pengine kumpa yule asiyeistahili ama mpokea rushwa kujinufaisha tu mwenyewe. Kuna nyakati hata sheria hupindishwa kwa sababu ya rushwa. Umewahi kuombwa ama kutoa rushwa ili kupata huduma yoyote ile?
Unalifahamu vipi tatizo la Usonji?
Ugonjwa wa Usonji au Autism ni tatizo la kibaiolojia ambalo kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani, WHO, huathiri mtoto mmoja kati ya kila watoto 100 duniani. Dalili zake huanza kuonekana mapema sana, kuanzia umri wa miaka mitatu na kuendelea. Ni vigumu kugundua dalili zake. Lakini kwenye video hii unaweza kujifunza mengi.
Utafiti: Kiwango cha Umasikini Ujerumani bado kipo juu
Ripoti mpya ya makundi ya ustawi wa jamii Paritätischer Gesamtverband inaonyesha kuwa kiwango cha umaskini nchini Ujerumani bado kipo juu. Takwimu za hivi karibuni zinaonyesha kuwa asilimia 16.8 ya watu wanaishi katika umasikini, hiyo ikiwa ni takriban watu milioni 14.2. Kwa mujibu wa ripoti hali ya umasikini imewaathiri watoto pamoja na kundi la wastaafu.
Wasichana wanavyosherehekea sikukuu ya Pasaka
Katika sikukuu ya pasaka kumekuwa na changamoto nyingi ambazo huwakuta wasichana pale wanapoenda kujivinjari katika viwanja tofauti tofauti lakini vipi wanaweza kuepukana na hayaWasichana wanavyosherehekea sikukuu ya Pasaka
Programu ya simu DigiCow yaleta mapinduzi kwa wafugaji
Peninah Njeri ambae anazitambua changamoto zinazowakabili wafugaji wa ngo'ombe wa maziwa nchini Kenya, ameunda jukwaa la kidijitali ambalo linatoa habari na rasilimali muhimu katika masuala ya ufugaji. DigiCow, imeleta mapinduzi makubwa kwa wafugaji na sasa takriban wafugaji 60,000 barani Afrika wanategemea jukwaa hilo kwa ufugaji wa kisasa.
Joto kali lina athari gani mwilini ?
Daktari Jalab Ashraf atowa maelezo zaidi jinsi ya kuhakikisha tunabakia imara kiafya katika kipindi hiki cha joto kali.
Wimbo ´Supa Woman´ waibua harakati za wanawake Msumbiji
Kibao ´Supa Woman´ cha mwanamuziki na mwanaharakati wa Msumbiji Katia Vanessa kimeibua vuguvugu la kuwainua wanawake.
Nini tathmini ya 'furaha' kwako?
Je wewe ni mtu mwenye furaha? Una furaha kiasi gani? Furaha ina thamani gani kwako?
Kivuli cha Ukoloni wa Ujerumani - Sehemu ya Kumi
Katika sehemu ya 10 ya simulizi tunatizama jinsi migogoro ya mipaka inayoshuhudiwa leo nchini Cameroon, Namibia na Tanzania ilivyo na mizizi yake toka enzi ya ukoloni.
Kivuli cha Ukoloni wa Ujerumani - Sehemu ya Tisa
Katika makala hii tunaangalia jinsi wakoloni wa kijerumani walivyotumia nadharia ya rangi tofauti za binadamu ili kuhalalisha udhalimu wa ukoloni wao.
Kivuli cha Ukoloni wa Ujerumani - Sehemu ya Nane
Kwa karne kadhaa sasa matibabu yaliyogunduliwa na mataifa ya magharibi yameokoa maisha ya mamilioni ya watu duniani. Lakini hali haikuwa hivyo katika siku za mwanzo mwanzo za ukoloni wa nchi za Ulaya barani Afrika.
Kivuli cha Ukoloni wa Ujerumani - Sehemu ya Saba
Mara hii tunamuangazia Quane Martin Dibobe, mwanaharakati wa haki za binadamu aliyepinga unyonyaji wa Ujerumani katika makoloni yake.
Kivuli cha ukoloni wa Ujerumani - Sehemu ya Sita
Kwenye sehemu ya 6 ya mfululizo wa simulizi tunaimulika miongo mitatu ya Utawala wa Ujerumani huko Togoland, koloni lililozingatiwa na viongozi mjini Berlin kuwa la mfano kuliko yote barani Afrika.
Kivuli cha Ukoloni wa Ujerumani - Sehemu ya Tano
Tunaendelea na mfululizo wa makala za kivuli cha ukoloni wa wajerumani barani Afrika ambapo hii leo tunaingia kwenye sehemu ya tano.
Kivuli cha Ukoloni wa Ujerumani- Sehemu ya Nne
Mara hii tunamulika mauaji ya kimbari yaliyofanywa na serikali ya ukoloni wa Wajerumani kati ya mwaka 1904 hadi 1908 dhidi ya makabila ya Herero na Nama huko Nambia, Kusini mwa Afrika.
Kivuli cha Ukoloni wa Ujerumani- Sehemu ya Tatu
Sikiliza sehemu hii ya tatu ya mfululizo wa makala zetu juu ya ukoloni barani Afrika.
Kivuli cha Ukoloni wa Ujerumani - Sehemu ya Pili
Sikiliza sehemu hii ya pili ya mfululizo wa makala zetu juu ya ukoloni barani Afrika.
Kivuli cha ukoloni wa Ujerumani - Sehemu ya Kwanza
Kufikia mwaka 1885, mfanyibiashara wa Ujerumani alifanikiwa kununua pwani nzima ya Kiafrika. Alifanya hivyo kwa kutumia bunduki chache alizokuwa nazo pamoja na mkataba wenye hila. Mkataba huo pamoja na mikataba mingine barani Afrika ilifuangua mwanya kwa utawala wa kikoloni wa Ujerumani.
Hisia za kutojiamini
Umewahi kupata hisia za kutojiamini? Wanasaikolojia wanasema hisia hizo huchangiwa na mambo tofauti ikiwemo malezi na tabia binafsi. #Kurunziafya inatizama hisia hizo, ambazo si ugonjwa lakini hutupata katika maisha yetu ya kila siku.
Wasichana jitokezeni kwenye sayansi na teknolojia
Miriam ameona ombwe la wasichana kujitosa katika masomo ya sayansi, kwa nafasi yake mbali na kuwa katika masuala ya sayansi na teknolojia, lakini pia amekuwa muhamasishaji kwa wasichana wengine kujitokeza katika sekta hiyo.
Uhaba wa mafundi Ujerumani, jee wahitaji kuwa na nini kuziwahi?
Zaidi ya watu milioni tano wanafanya kazi Ujerumani kama mafundi na wafanyabiashara. Lakini mwaka jana bado kulikuwa na nafasi za ajira 250,000 bila wafanyakazi. Je ungetamani kufanya kazi Ujerumani kama fundi au mfanyabiashara? Haya ndiyo mambo wahitaji kuwa nayo.
Ukurasa uliotangulia
Ukurasa 2 wa 6
Ukurasa unaofuatia