1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMali

Waasi nchini Mali wadai kudhibiti kambi ya kijeshi

5 Oktoba 2023

Waasi wa Tuareg wamesema hapo jana kuwa wamechukua udhibiti wa kambi ya wanajeshi wa Mali kaskazini mwa nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/4X7mP
Mali | Soldat mit Ak-47
Mwanajeshi wa Mali akiwa huko GaoPicha: KENZO TRIBOUILLARD/AFP/Getty Images

Mapigano yamekuwa yakiongezeka katika eneo hilo tangu mwezi Agosti mwaka huu, ambapo kambi kadhaa za jeshi kati ya Timbuktu na Gao zimekuwa zikishambuliwa.      

Baraza la Juu la Umoja wa Azawad  (CUA) limesema katika taarifa fupi kwenye mitandao ya kijamii kwamba kambi ya jeshi huko Taoussa, katika eneo la Gao, "iko chini ya udhibiti" wa waasi, bila hata hivyo kutoa maelezo zaidi.

Mwaka 2012, makundi hayo ya waasi yalianzisha uasi dhidi ya taifa la Mali kabla ya kutia saini makubaliano ya amani mwaka 2015. Desemba mwaka jana,  Uratibu wa Harakati za Azawad (CMA) ilitangaza kujiondoa na kuwashutumu watawala wa kijeshi kwa kukiuka makubaliano hayo.