1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kusini

Wafuasi wa Yoon wavamia Mahakama ya Korea Kusini

19 Januari 2025

Mamia ya wafuasi wa Rais wa Korea Kusini aliyekamatwa, Yoon Suk Yeol, wamevamia majengo ya mahakama na kufanya uharibifu wa kuvunja madirisha na vifaa vyengine mapema leo Jumapili.

https://p.dw.com/p/4pL4Q
Korea Kusini -Kukamatwa kwa Yoon Suk Yeol
Wafuasi wa rais wa Korea Kusini aliyekamatwa wavamia Mahakama.Picha: Ahn Young-joon/AP/picture alliance

Vurugu hizo zimejiri muda mfupi baada ya mahakama kutangaza uamuzi wa kuendelea kuzuiliwa rumande  kwa rais Yoon.

Video zimeonyesha waandamanaji wakitumia vifaa vya kuzima moto dhidi ya  polisi waliokuwa wakilinda mlango wa mbele wa Mahakama hiyo, kabla ya kufuliza ndani, kuharibu vifaa vya ofisi.

Soma pia: Mahakama ya Korea Kusini yakataa Rais Yoon kuachiwa huru

Kaimu rais Choi Sang-mok, katika taarifa yake amesema serikali imesikitishwa na matukio ya ukiukaji sheria na vurugu akisema matukio hayo hayakutarajiwa katika taifa hilo la kidemokrasia.

Polisi walirejesha utulivu saa chache baadaye, na kuwakamata waandamanaji 46 na kuahidi kuwasaka wengine waliohusika.