Rishi Sunak kukutana na Kansela Scholz nchini Ujerumani
24 Aprili 2024Matangazo
Ziara hiyo ilikuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu na inatazamiwa kuimarisha ushirikiano wa usalama baada ya London kutangaza hatua ya kuongeza matumizi ya ulinzi.
Kulingana na taarifa kutoka kwa serikali ya Uingereza, viongozi hao wawili wanatarajiwa kutangaza mipango ya ushirikiano wa kijeshi kwa kuendeleza udhibiti wa mifumo ya makombora na pia kujadili kuhusu masuala ya uwekezaji na miradi ya nishati.
Sunak ambaye alikuwa hajafanya ziara rasmi nchini Ujerumani tangu aliposhikilia wadhifa wa Waziri Mkuu wa Uingereza mnamo Oktoba mwaka 2022, alipunguza safari zake za kimataifa na kukabidhi sehemu kubwa ya majukumu ya kidiplomasia kwa Waziri wake wa Mambo ya Nje David Cameron.