SiasaKorea Kusini
Waziri wa zamani wa ulinzi wa Korea Kusini akamatwa
9 Desemba 2024Matangazo
Hatua ya kukamatwa kwa kiongozi huyo ni kutokana na jukumu lake katika sheria ya kijeshi iliyotangazwa na Rais Yoon Suk Yeol, ambaye amenusurika kuondolewa madarakani kwa kura ya kutokuwa na imani naye Bungeni.
Hata hivyo kiongozi wa chama kikuu cha upinzani huko Korea Kusini Lee Jae-myung, amesema chama hicho kitajaribu tena Desemba 14 kumuondoa madarakani rais Yoon Suk Yeol, kufuatia hatua yake ya kutangaza sheria ya kijeshi.
Ripoti za vyombo vya habari nchini humo zinaeleza kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Lee Sang Min, ambaye ni mshirika wa karibu
wa Rais Yoon Suk Yeol, amejiuzulu wakati mzozo wa kisiasa ukiendelea kufukuta nchini humo.