1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wizara ya Afya Gaza yasema idadi ya vifo imeongezeka

29 Desemba 2023

Israel imeendeleza mashambulizi yake katika Ukanda wa Gaza na kusababisha maafa makubwa. Kulingana na wizara ya afya inayodhibitiwa na Hamas, watu 187 wameuawa kwa siku moja huku idadi ya vifo ikifikia 21,507.

https://p.dw.com/p/4aiZP
Ukanda wa Gaza | Jitihada za kutafuta miili katika vifusi zikiendelea
Wakaazi wa Gaza wakiendelea kutafuta miili ya waliofukiwa na vifusi, baada ya mashambulizi ya israel Ukanda wa Gaza.Picha: Mohammed Talatene/dpa/picture alliance

Wizara hiyo imeongeza kuwa Wapalestina wengine zaidi ya 50,000 wakiwa wamejeruhiwa. Mkurugenzi wa hospitali ya Abu Youssef al-Najjar, Marwan al-Hams amesema, bado kuna takriban wengine 10,000 wakiwa chini ya vifusi.

Hayo yakijiri, viongozi wa kundi la Hamas wanatarajiwa mjini Cairo nchini Misri kwa mazungumzo.

Soma pia:Israel yaongeza mashambulizi ya anga na ardhini Gaza

Leo hii pia, Jeshi la Israel limefahamisha kuwa watu wanne wamejeruhiwa kusini mwa mji wa Hebron katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kimabavu baada ya Mpalestina mmoja kuwagonga watu kwa gari karibu na kituo cha jeshi.