1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiIndia

Yellen hafikirii kuwa uchumi wa Marekani utashuka

17 Julai 2023

Waziri wa Fedha wa Marekani, Janet Yellen, amesema leo kwamba nchi yake inapiga hatua nzuri katika kupunguza mfumuko wa bei na hatarajii kushuka kwa uchumi wa taifa hilo kubwa duniani.

https://p.dw.com/p/4U0fI
Indien Gandhinagar | vor G20-Treffen der Finanzminister | US-Finanzministerin Yellen
Picha: SAM PANTHAKY/AFP

Akizungumza na televisheni ya Bloomberg ya India wakati wa mkutano wa maafisa wa fedha wa mataifa ya kundi la G20, Yellen amesema ukuaji wa kasi ya chini nchiniChina huenda ukaenea katika chumi nyingine lakini uchumi wa Marekani uko katika mwelekeo sahihi.

Mapema baada ya mazungumzo ya pande mbili na Waziri wa Fedha wa India, Nirmala Sitharaman, pembezoni mwa mkutano huo wa G20.

Soma Pia:Mkutano wa wakuu wa fedha waanza nchini India

Yellen amesema ni muhimu kushughulikia mahitaji ya harakaya kuongeza uwezo wa benki wa kutoa mikopo kwa masharti nafuu na kuzisaidia nchi za kipato cha chini ili ziimarishe juhudi zao. Ushirikiano na India katika juhudi hizi litakuwa suala muhimu katika ufanisi wake.

Yellen ameongeza kuwa mataifa hayo mawili yanakaribia kuafikia makubaliano kuhusu mfumo wa kodi ya kima cha chini duniani.