Mlinzi wa Macron Mahakamani kwa kuwapiga waandamanaji
13 Septemba 2021Macron, ambaye aliufanya uadilifu kuwa swala la msingi katika Kampeni zake wa mwaka 2017, alilazimika kumtimua mlinzi wake Alexandre Benalla baada ya kuibuka kwa video iliyomuonesha akishambulia kijana mmoja na kumkaba koo msichana mmoja wakati wa maadamano ya kupinga ubepari mjini Paris.
Mlinzi huyo wa zamani mwenye umbo la kibondia, ambaye sasa ameifikisha miaka 30, alionekana akiwa amevalia sera rasmi za kazi hata ingawa alikua likizoni, na kuruhusiwa tu kuhudhuria maadamano hayo kama mtazamaji.
Uongozi wa Rais Macron ililaumiwa kwa hatua ya kujaribu kuficha yaliojiri na kushindwa kumchukulia hatua za kisheria mlinzi huyo hadi gazeti mmoja ya Ufaransa Le Monde, kuibuka na ushahidi kwenye video, miezi miwili baada ya tukio.
Kadhia hiyo ya "Benallagate" ilikuwa na kuwa mtihani wa kwanza mkubwa katika uongozi wa Macron ambaye alijishinda urais kwa hadi ya kurejesha uongozi bora".
Serikali yake ilinusurika kura mbili za kutokuwa na imani nayo bungeni. Licha ya hayo kamati ya uchuguzi ya Senati ambayo iliwahoji wasaidizi wa Macron ilibaini kasoro kubwa katika namna serikali ilivyoshughulikia uchunguzi wa tukio hilo.
Benalla alishtakiwa kwa madai ya kupigana na vile vile kujaribu kuingilia masuala ya Polisi bila idhini.
Soma pia: Macron apatikana kwenye orodha ya udukuzi
Mlinzi huyo wa zamani, ameyakanusha mashtaka hayo, huku akisema aliwajibika kwa hali ya kihisia kwa nia mahususi ya kujaribu kusaidia maafisa wa polisi kuwakamata waadamanaji waliotoa vurugu.
Mshtakiwa mwingine pia ni rafiki wa Benalla, Vincent Crase, mkuu wa zamani wa usalama katika chama cha mrengo wa kati cha Macron. Crase pia alipigwa picha akiwazuia kwa kutumia nguvu waandamanaji hao.
Maafisa wawili wa polisi, wanaotuhumiwa kumpa Benalla mkanda wa video ya uchunguzi, katika juhudi za kudai kuwa matendo yake yalikuwa halali, pia wanashtakiwa.
Wakili wa Benalla amekataa kuongea na wanahabari kabla ya kesi hiyo.
Wapenzi hawo wawili ambao walishambuliwa na Benalla katika tukio hilo, walishtakiwa pia kwa madai ya kuirushia polisi vitu, kosa ambalo lilipelekea kutozwa faini ya Euro 500.
Soma pia:Macron, Le Pen wakashifiana hadharani
"Kukamata mtu anayetenda uhalifu hakuadhibiwi kisheria," wakili wa Crase Christian Saint-Palais alihoji, akisema mteja wake alifanya kitendo hicho katika hali ya kukabiliana, kwa haraka na yaliokua yakitendaka.
Benalla alianza kumfanyia kazi Rais Macron kama mlinzi mnamo 2016. Alipandishwa wadhifa Mei 2017 baada ya ushindi mkubwa wa Macron, huku akionekana kujitokeza kama mwaandani wa karibu wa kiongozi huyo wa Ufaransa.
"Alionenekana kama mtu aliyeweza kutatua shida zote kwa hali ya ufanisi" afisa mkuu wa zamani wa kampeni hizo za Macron alisema.
Benalla alipata marupurupu ambayo kawaida hupatiwa maafisa wakuu wa utawala. Mlinzi huyo alitengewa nyumba karibu na kasri la Elysee anakoishi rais, pia alikuwa na ruhusa ya kuingia Bunge la Kitaifa. Isitoshe alikonekana kulitumia eneo la zoezi lilotengewa maafisa wakuu wa kiserikali.
Soma pia: Wafaransa kumchagua Rais mpya kati ya Macron na Le Pen
Baada ya kashfa hiyo, Benalla pia alikiri kubeba bunduki wakati wa safari na Macron, ingawa alikuwa ameruhusiwa tu kuwa nayo ndani ya makao makuu ya chama cha Macron.
Bado haijulikani wazi alikokitoa kofia ya polisi ambayo alionekana amevaa wakati wa shambulio la Mei Mosi.
Wachunguzi waligundua kwamba aliendelea kutumia pasipoti za kidiplomasia kwa safari za Afrika na Israeli, ambapo anaaminika alijaribu kuunda biashara ya kibinafsi.
Benalla pia anashukiwa kutumia hati bandia kupata mojawapo ya pasipoti zake, mashtaka ambayo ameyakana.
Benalla pia atakabiliwa na shtaka la kubeba bunduki kinyume cha sheria, kulingana na picha yake katika mkahawa mmoja.