Watu 15 wauwawa Syria
4 Januari 2021Shirika la uangalizi wa haki za binaadam nchini Syria, limeripoti kuwa wanajeshi na washirika wao wa kivita 12, raia watatu na mtoto mmoja wameuwawa na wengine 15 kujeruhiwa. Soma zaidi Waangalizi: Israel yashambulia Syria na kuua wapiganaji 8
Ripoti ya shirika la habari la Syria SANA imesema kuwa shambulizi hilo la "Kigaidi" limewauwa raia 9.
Shambulizi jengine
Wiki iliyopita, Disemba 30, kundi hilo linaojiita Dola la Kiislamu lilitangaza kuhusika katika shambulizi jengine la basi katika mkoa wa Deir al-Zour Mashariki mwa Syria na kusababisha vifo vya wanajeshi wasiopungua 30 wa serikali. Soma zaidi Waasi 78 wauawa Syria
Kulingana na uchuguzi wanajeshi waliouwawa walikuwa njiani kuelekea nyumbani kwao kwa likizo ya Mwaka Mpya.
Kikundi hicho kilikabiliwa mnamo Machi 2019, lakini bado kinaendelea kufanya mashambulizi katika jangwa lilipo Badia, eneo ambalo linapatikana katikati mwa Syria mashariki, kuelea katika mpaka na Iraq.
"Kundi hilo tangu wakati wa msimu wa mapukutiko uliyopita lilikuwa likiimarisha shughuli zake na kuanzisha mashambulizi dhidi ya vikosi vya serikali huko Badia," amesema mkuu wa shirika la Uangalizi Rami Abdel Rahman. Soma pia UN:Wapiganaji wa IS bado wanaendelea na operesheni zao
Dola la Kiisilamu lilipoteza maeneo mengi na kushindwa katika operesheni za kijeshi huko Syria na Iraq katika miaka miwili iliyopita. Lakini washirika wake mara kwa mara wanaendelea kufanya mashambulizi katika nchi zote mbili.
Vyanzo: AFPE/DPAE