UN:Taliban ibadili misimamo yake dhidi ya wanawake
28 Desemba 2022Baraza hilo la Umoja wa Mataifa lenye wananchama 15 limesema katika taarifa yake kwamba limeshtushwa na ongezeko la vikwazo vya elimu kwa wanawake na kutoa wito wa ushiriki kamili wa wanawake na wasichana katika taifa hilo la Asia ya kati.
Baraza hilo limeutaka utawala huo ambao umekuwa namkururo wa vikwazo dhidi ya wanawake kufungua shule kwa wasichana na kubadili sera na mwenendo ambao unaongeza mmomonyoko wa haki za binadamu na uhuru wa kimsingi.
Katika taarifa hiyo imegusia pia marufuku ya wanawake kufanya kati katika mashirika yasio ya kiserikali na kuelezea matokeo mabaya zaidi kwenye oparesheni za misaada ya kiutu katika taifa hilo masikini, linalotegemea misaada.
Vikwazo hivi vinakinzana na ahadi zilizotolewa na utawala wa Taliban kwa watu wa Afghanistan pamoja na matarajio ya Jumuia ya Kimataifa. ilisema sehemu ya ripoti hiyo.
Soma pia:Taliban wakosolewa na EU
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameunga mkono ujumbe wa Baraza la Usalama, akitaja vikwazo vya hivi karibuni zaidi kwa wanawake na wasichana kama ni ukiukwaji wa haki za binadamu usio vumilika na lazima kubatilishwa mara moja.
Haki za wanawake sharti muhimu kwa Taliban
Jumuia ya kimataifa imekuwa ikiheshimu na kutoa kipaumbele juu utambuzi wake na kurejeshwa kwa misaada ya kiutu, huku haki za wanawake ikilifanya sharti muhimu katika mazungumzo na serikali ya Taliban.
Mapema jana Jumanne ,Kamishna Mkuu wa haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Turk, alionya juu ya kile alichokiita matokeo mabaya yatakayosababishwa na sera hizo.
"Hakuna nchi inayoweza kuendelea kijamii na kiuchumi huku nusu ya watu wake wakitengwa." Alisema mkuu huyo wa haki za binadamu.
Soma pia:Uturuki, Saudi Arabia walaani msimamo wa Taliban
Vikwazo hivi visivyoeleweka vilivyowekwa kwa wanawake na wasichana sio tu vitaongeza mateso ya Waafghanistan wote.
"Nahofia, vitaleta hatari nje ya mipaka ya Afghanistan." Ilisema taarifa hiyo iliofikia vyombo vya habari.
Turk alionya kuwa kupiga marufuku wanawake kufanya kazi katika mashirika yasiyo ya kiserikali kutazinyima familia zao mapato hasa wakati huu mahitaji ya kibinadamu yameongezeka.
Aidha taarifa yake inamulika pia namna ambavyo mashirika ya kiraia yatavyodhoofika katika kufikia malengo yake.
"kudhoofisha kwa kiasi kikubwa, ikiwa sio kuharibu uwezo wa mashirika kutoa huduma muhimu."
Hali ya uhutaji wa wakaazi Afghanistan
Afisa wa ngazi za juu wa misaada Umoja wa Mataifa Martin Griffiths, ameliambia baraza la Isalama la Umoja wa Mataifa wiki iliopita kwamba asilimia 97 ya waafghanistan wanaishi kwenye umasikini.
Theluthi mbili ya watu wanahitaji misaada kwa ajili ya kuishi huku wengine milioni 20 wakikabiliwa na hali mbaya ya njaa.
katikati ya lindi la uhitaji mkubwa wa mahitaji muhimu kundi la wasichana wapatao milioni 1.1, lilipata pigo kupigwa marufuku kuhudhuria shule.
Soma pia:UN: Wanawake na watoto waliuwawa zaidi Afghanistan
Katika pigo lingine la hivi karibuni dhidi ya haki za wanawake nchini Afghanistan tangu kundi la Taliban kutwaa tena mamlaka mwaka jana, watawala hao wenye msimamo mkaliwalipiga marufuku wanawake kufanya kazi katika mashirika yasiyo ya kiserikali, na hivyo kupata ukosoaji mkubwa kutoka jumuiya ya kimataifa.
Mashirika kadhaa ya kimataifa yanayoendesha shughuli zake nchini humo siku ya Jumapili yalitangaza kisitisha shughuli zao nchini humo kwa kile walichosema, itakuwa vigumu kuyafikia baadhi ya makundi ikiwemo wanawake na watoto wanaohitaji misaada.