You need to enable JavaScript to run this app.
Nenda kwenye maudhui
Nenda kwenye orodha kuu
Nenda tovuti zaidi za DW
Vidio zetu
Sauti zetu
Maeneo
Tanzania
Kenya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Afrika
Ulaya
Mada
Haki za binadamu
Mazingira
Afya
Teknolojia
Kategoria
Matukio ya Kisiasa
Masuala ya Jamii
Michezo
Sauti zetu
Vidio zetu
Yanayoangaziwa
Uchaguzi wa Marekani 2024
Mzozo wa Israel na Hamas
Bundesliga
Matangazo
Picha: DW
Picha: DW
Vidio zetu
Tazama vidio zetu hapa
Ruka sehemu inayofuata Maudhui yote kwenye mada hii
Maudhui yote kwenye mada hii
Kirchmesse: Sherehe za kitamadauni Ujerumani
Sherehe hizi zimekuwa zikifanyika kwa miaka na dahari sasa, ambapo zinawaleta pamoja wajerumani.
Msanii wa michoro ya Mandala mjini Mombasa
Mariam Suleiman, ni msanii aliyeinuka kwa juhudi zake mjini Mombasa kwa michoro ya kuvutia ya Mandala.
Kurunzi Afya: Chanjo ya uraibu wa cocaine
Wanasayansi nchini Brazili, wako mbioni kutengeneza chanjo ya kutibu uraibu wa dawa za kulevya. Chanjo hiyo iliyopewa jina la Calixcoca tayari imeonyesha mafanikio katika majaribio kwa yaliyofanywa kwa Wanyama.
Nguo zilizotengenezwa kwa rangi za taka za chakula, Kenya
Kampuni ya nchini Kenya inayotengeneza nguo za wanawake pekee, inafafanua upya mtindo kwa kuunda mavazi kutumia rangi za matunda na mboga zinazotokana na taka za chakula.
Mtanziko wa Ujerumani juu ya azimio la Umoja wa Mataifa
Ujerumani inapenda kujiona kama taifa lenye ushawishi wa kidiplomasia ulimwenguni. Lakini hatua yake ya kutopiga kura katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa juu ya azimio la usitishwaji vita katika mzozo wa Israel na Hamas kumeiweka Berlin katika mtanziko mkubwa.
Ulemavu si mwisho wa maisha
Licha kwamba wao ni walemavu wa viungo, hawajaruhusu hali hiyo kuwa kisiki au kuwapotezea matumaini ya kucheza mpira wa kikapu. Hapa wako uwanjani wakifanya mazoezi mjini Bukavu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Ndoto yao ni kupiga hatua zaidi na kushiriki michezo ya kitaifa na kimataifa. Mitima Delachance aliwatembelea na anasimulia zaidi
Je vijana wana uelewa tosha na ushiriki kamili kukabili athari za mabadiliko ya tabia nchi?
Ulimwengu unapofanya juu chini kukabili athari za mabadiliko ya tabia nchi swali linaloibuka wakati mwingine ni kuhusu uelewa na ushiriki wa vijana. Je wameshirikishwa vya kutosha? Na je mchango wao ni upi? Mwandishi wetu wa Arusha Veronica Natalis anaangazia kauli ya baadhi ya vijana na juhudi zao katika suala hilo zima. Tizama
Teknolojia ya viungo bandia
Teknolojia inaenda kwa kasi sana. Hii leo mtu mwenye ulemavu anaweza kupewa mkono unaotumia umeme. Hauna tofauti sana na mkono wako wa kawaida kwa sababu mkono huu una uwezo wa shughuli mbalimbali. Hebu tujiunge na Tatu Yahya aliyeshuhudia haya kwa macho. #kurunziafya
Ummi Sadick, msichana jasiri anayeongoza kampeni ya afya
Kutana na Ummi Sadick, msichana anayeongoza kampeni ya afya ya jamii mjini Mombasa, pwani ya Kenya.
Kurunzi Ujerumani - Soko la Mayai Ujerumani
Ujermani inazalisha asilimia 15.1 ya mayai yote katika soko la Umoja wa Ulaya. Kwa wastani, kila Mjerumani hula mayai 23
Juhudi za kukomesha ukeketaji wasichana na wanawake
Kadhia ya ukeketaji wa wasichana na wanawake ingali inafanywa kisirisiri miongoni mwa baadhi ya jamii za Afrika. Mashirika ya kimataifa na watunga sera mbali mbali barani humo wanahimiza sera na sheria kali kutungwa kukabili kadhia hiyo.
Mwanamke wa kwanza kupata shahada jamii ya Hamer, Ethiopia
Goito aliyekulia katika jamii ya wafugaji nchini Ethiopia alijizatiti na kuwa mwanamke wa kwanza kupata shahada katika jamii yake ya Hamer.
Ni kwa nini Kenya imejitokeza kupeleka polisi wake Haiti?
Mahakama ya Kenya imezuia kwa muda mipango ya serikali ya kupeleka maafisa wa polisi nchini Haiti kusubiri kusikilizwa kwa kesi iliyowasilishwa. Wawasilishaji hoja wanasema uamuzi wa kupeleka jeshi ni kinyume na katiba. Kenya ilijitolea kuwatuma polisi wake Haiti, taifa lililoharibiwa na uhalifu wa magenge yenye silaha. Je, ni kwa nini Kenya imejitolea kuwatuma polisi wake Haiti?
Uboreshaji wa mpangilio wa meno kinywani
Kuwa na meno yaliyopangika vizuri huweza kukuongezea ujasiri unapozungumza na pia kufanya tabasamu lako liwe la kuvutia. Kinyume chake ni kwamba unaweza kupoteza ujasiri unapozungumza, unapotabasamu au unapocheka. Je unawezaje kuboresha mpangilio wa meno yako? Tazama vidio hii ya Kurunzi Afya.
Msichana Jasiri: Mfahamu Ahlam Swaleh, binti anayewasaidia vijana kuleta mabadiliko
Ni binti aliyejitokeza kuwasaidia vijana wenzake kuleta mabadiliko kupitia mpango wa ushauri kwa wanafunzi. Ni binti wa miaka 24 tu, lakini tayari ananuia kufanya mabo makubwa sana katika kuwainua wenzake huko pwani ya Mombasa nchini Kenya. Ni nani huyu? Ungana na Fathiya Omar kumfahamu zaidi kupitia makala haya ya msichana Jasiri.
Silke: Nimepewa moyo na mapafu kutoka kwa mfadhili nisiemjua
Maisha ya Silke Schulze yamenusurika baada ya kupata moyo na mapafu kutoka kwa mchangiaji alieidhinisha kuondolewa viungo vyake punde tu baada ya kufariki, mfumo huo umesaidia watu wengi waliokuwa wanahitaji msaada, sasa anaishi kwa kushuru kwa hisani isio mithilika.
Mfahamu Mai Zumo msichana muigizaji
Mai Zumo alingia kwenye sanaa ya uchekeshaji akiwa na miaka mitatu, safari yake ilianza bila ya kutaraji.
Mauti harusini- Iraq yaomboleza vifo vya zaidi ya watu 100
Iraq inaomboleza vifo vya karibu watu 100 waliopoteza maisha kwa mkasa wa moto uliozuka kwenye ukumbi wa harusi kaskazini mwa nchi hiyo usiku wa kuamkia Jumatano. Bwana na bi harusi ni miongoni mwa waliouawa.
Wakaazi Abidjan waweka mifumo ya maji taka kulinda afya
Taka imekuwa ni kero kubwa na kuhatarisha afya ya jamii katika moja ya kitongoji katika mji wa kiuchumi Ivory Coast Abidjan, kundi la vijana limeamua kutosubiri mamlaka kuchukua hatua, wameamua kutengeneza mifumo ya maji taka ili kuondoa tatizo kadhalika kuleta ustawi wa afya ya jamii katika eneo husika.
Msichana Jasiri inamuangazia dada mjenzi Dar es Salaam
Recho ni msichana aliye amua kuipigania kesho yake licha ya baadhi ya watu kuwa na mtazamo tofauti juu yake lakini haikuwa sababu ya yeye kutokufika hapa alipo. #MsichanaJasiri
Ghana: Mavazi na vifaa vingine kutokana na taka za plastiki
Hebu fikiria jinsi taka za mifuko ya plastiki zimezagaa kwingi katika baadhi ya mitaa na miji. Kule Kaskazini mwa Ghana, kundi moja la kina mama limeamua kuzitumia taka hizo kama malighafi kushona vifaa vya wanafunzi ikiwemo kofia, jaketi na makoti ya kujikinga dhidi ya mvua. Wanapofanya hivyo wanasaidia kuondoa uchafu na kuacha mazingiza ikiwa safi. Hebu tizama kisha utuambie umeionaje?
Shimoni:Nguvu ya filamu ndani ya mwanamke
Tamasha la Filamu za Kiafrika la Köln linafanyika kwa mara ya 20, Angela Wanjiku Wamai mtengenezaji wa filamu kutoka Kenya anaonesha filamu yake kwa mara ya kwanza katika jukwaa hilo la kimataifa, filamu yake inaonesha na kutambua mapambano ya mtu mmoja mmoja kwenye jamii katika kuleta mabadiliko.
Msichana Jasiri: Unaitumiaje mitandao ya kijamii?
Katikati ya changamoto zinazotokana na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii, nchini Tanzania anajitokeza binti huyu ambaye anawasaidia wengi kutambua ya kwamba mitandao hii si ya kupotezea muda, bali ina faida. Ni kwa namna gani? Ungana na Tatu Yahya anayetukutanisha na binti huyu katika makala ya Msichana Jasiri.
Fahamu zaidi kuhusu homa ya baridi ya bisi
Homa kali ya baridi ya bisi au rumatizimu kitaalamu 'rheumatic fever' ni ugonjwa ambao husababishwa na bakteria aina ya steptococcs matokeo yake huwa ni kushambuliwa kwa viungo kama vile kiwiko na magoti hivyo hupelekea baadhi yao kuharibika au kuziba kwa mishipa ya moyo.
Msichana Jasiri: Wachezaji chipukizi wa mpira wa kikapu
Michezo sasa imegeuka fursa kwa vijana na hata wasichana pia hawajabaki nyuma katika kuitumia michezo kukutana na watu na kufika mbali zaidi, licha ya kuwa na changamoto katika michezo na jamii kuwa na mtazamo mbaya juu yao, lakini si sababu ya wao kutokuziishi ndoto zao. Je wamefanikisha katika hili?
Khadija Sultan anavyotumia nguvu ya mitandao kwenye biashara
Nguvu ya mitandao ya kijamii ilimpa fursa ya kujielimisha na kuanzisha bidhaa yake kwa ajili ya nywele, Katika kufikia lengo la ubora alifanyia kazi maoni hasi kuliko chanya. Tazama video hii ya msichana jasiri kisha tuambie katika kufikia lengo vipi unafanyia kazi maoni hasi?
Mfahamu Carol Mkenya anayemiliki mgahawa Ujerumani
Carol-Waithira Mühlenbrock alikulia nchini Kenya na kusoma chuoni huko. Alikuja Ujerumani miaka 17 iliyopita na kuanza upya kujenga maisha. Leo, yeye ni mmiliki wa mgahawa, mpishi mkuu na anaeneza mapishi yake pamoja na uzoefu wake kupitia mitandao ya kijamii. Katika video hii, anazungumzia jinsi alivyofikia mahali alipo leo na jinsi mtazamo wake kuhusu anachokiona kama “nyumbani” umebadilika.
Wanawake wanapoamua kujifunga kizazi
Jasmin mwenye umri wa miaka 25 alifungwa kizazi kwa sababu hataki kupata watoto. Lakini kupata daktari ambaye angefanya upasuaji haikuwa rahisi.Je mbinu gani alitumia? Tazama video
Mikopo na madhila yake
Ulishawahi kukumbwa na maswahibu ya mikopo? Kwamba ukakopa halafu kurudisha ikawa changamoto? Yapi yalikukumba? Hebu tuambie hapa, baada ya kutazama video ya kina mama hawa.
Madaktari wa Sudan waanzisha kliniki Chad kuwatibu wahamiaji
Madaktari wa Sudan ambao pia ni wahamiaji walioko kambini Chad baada ya kukimbia mapigano makali Darfur wajitolea kuyaokoa maisha ya wagonjwa kambini. Huo ndio ubinadamu. Tizama kwenye KurunziAfya.
Jinsi kampuni ya mpira inaboresha maisha ya walemavu Kenya
Kampuni ya Alive and Kicking inayotengeneza mipira ya michezo imeongeza idadi ya watu wenye ulemavu kuwa wafanyakazi wake kiwandani. Kampuni hiyo inasema huo ni mchango wake kufikia malengo ya maendeleo endelevu ya jamii.
Upinzani Zimbabwe wapinga matokeo ya uchaguzi wa rais
Chama kikuu cha upinzani nchini Zimbabwe cha Citizens Coalition for Change (CCC) kinachookozwa na Nelson Chamisa, kimetangaza msimamo wa kuyapinga matokeo ya uchaguzi, siku moja tu ya baada ya Tume ya Uchaguzi ya taifa hilo kumtangaza Rais Emmerson Mnangangwa kuwa mshindi wa uchaguzi huo uliofanyika Jumatano na Alhamisi wiki iliyopita.
Meli ambayo pia ni maktaba yatia nanga Mombasa
Meli ya MV LOGOS HOPE husafiri kote ulimwenguni kutoa msaada wa elimu, maarifa na matumaini. ndani yake ni maktaba yenye zaidi ya vitabu 5,000 kwa manufaa ya wasomaji wanaoitembelea. Meli hii inayomilikiwa na shirika lisilo la serikali la GBA la Ujerumani itakuwa Mombasa kwa siku 45 na kisha kuelekea Dares salaam, Tanzania baadae hadi Afrika Kusini. Fathiya Omar anasimulia zaidi. #Kurunzi #MeliMak
Juhudi za kudhibiti uchafuzi wa plastiki Dar es Salaam
Kuna jitihada za kupunguza madhara ya plastik Tanzania ikiwemo kupiga marufuku mifuko ya plastiki, vijana wakusanyao taka za plastiki nao wana mchango katika kusaidia kutokutapakaa kwa plastik. Vijana wa kundi la Chatafisha miongoni mwa vijana kutoka Tanzania wanaosambaza elimu ya kudhibiti taka za plastiki katika ngazi za vyuo na katika mitaa.
Jumba la makumbusho la Kariandusi, Nakuru
Jumba la makumbusho la Kariandusi limesheni mabaki ya uvumbuzi wa kijiolojia, korongo na sanaa za utamaduni wa kale.
Urusi yalaumiwa kwa kifo cha mkuu wa Wagner
Wachunguzi wa ajali ya ndege leo wamechukua mabaki ya ndege hiyo na wameanzisha uchunguzi wa jinai.
Maajabu ya Koblenz
Mji wa Koblenz unafahamika kuwa moja ya miji ya kitalii nchini Ujerumani kutokana na uwepo wa vigari vya kuning'inia.
Ufahamu ugonjwa wa Dyslexie ambao huwapata watoto
Dyslexia ni tatizo la afya linalowapata baadhi ya watoto ambao hupata changamoto kutambua herufi zinazounda maneno na baadhi ya namba, baadhi ya wazazi hufikiri watoto hawana kumbukumbu nzuri.
Barabara kuu na kasi nchini Ujerumani
Kuna nchi kadhaa duniani ambazo hazina ukomo wa mwendo kasi barabarani, Ujerumani ni mojawapo ya hizo nchi. Mwandishi wa
Mtetezi wa sokwe Tanzania
Mfahamu mwanamama au shoshi au kikongwe mwanaharakati wa kumtetea sokwe na mazingira aliejikita kumtafiti sokwe na kuleta ustawi wa mnyama huyo aliehatarini na maradhi na kuvamiwa na shighuli za binadamu huko katika msitu wa gombe kigoma.
Maandalizi ya nusu fainali ya Kombe la Dunia la Wanawake
Michuano ya Kombe la Dunia la Wanawake 2023 inayoandaliwa Australia na New Zealand inaingia hatua ya nusu fainali.
Konokono ana faida jamani!
Mwanamama huyu anasema anafaidika kwelikweli na ufugaji wa konokono. Anawatumiaje? Mimi sisemi mengi, tizama video hii umsikie mfugaji huyu wa konokono. #kurunzi
Tanzania yafanya tamasha la kwanza la muziki wa Jazz
Ni tamasha la Kwanza la muziki wa Afro Jazz Tanzania lililopewa jina Evergreen Afro Jazz ambalo limewakusanya wasanii vijana wanaowika katika muziki huu, dhamira ikiwa kuuhuisha baada ya muziki huu kuonekana kana kwamba unatoweka. Tizama muziki mtamu kabisa wenye mahadhi ya Kiafrika. #kurunzi
Msichana Jasiri: Binti mwandishi wa vitabu
Ni binti mdogo sana, lakini tayari anaandika vitabu vyake anapokwenda safari mbalimbali. Ni nani huyu hasa? Ungana na Hadija Halifa aliyemtembelea binti huyu. Utafurahi kumsikiliza. #msichanajasiri
Mji wa Ujerumani ulioachwa wageuzwa makaazi ya wahamiaji
Kuzibua mishipa ya damu miguuni
Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali, asilimia 20 ambayo ni sawa na watu milioni 230 ulimwenguni kote, hupata tatizo la kuziba kwa mishipa ya damu ya miguu. Je chanzo, dalili ni zipi? Na matibabu? Kurunzi Afya inaangazia tatizo hilo la kiafya.
Tamasha kubwa duniani la muziki wa Rock laanza mjini Wacken Ujerumani
Tamasha kubwa zaidi la muziki wa Rock limeanza nchini Ujerumani. Ni tamasha linalohudhuriwa na zaidi ya watu 80,000 ila mwaka huu, hali mbaya ya hewa imepelekea idadi kudhibitiwa. Je, uko radhi kucheza matopeni ili umuone mwanamuziki unayempenda? Hebu watazame hawa Wajerumani.
Usafirishaji haramu wa binaadamu watishia watoto wa Afrika
Usafirishaji haramu wa watoto na unyonyaji unazidi kuongezeka katika njia ambayo hutumiwa na wahamiaji wasio na vibali wanapitia kutoka Pembe ya Afrika hadi Saudi Arabia. Umoja wa Mataifa umesema wavulana na wasichana wenye umri wa miaka 13 hadi 17 wako hatarini zaidi. #IOM
Msichana Jasiri, aliyerejea shule baada ya kujifungua
Huyu ndio tunamuita msichana jasiri. Hakutaka kuacha ndoto yake ipeperuke, akatumia fursa iliyotolewa na serikali ya Tanzania na kuamua kurudu shuleni baada ya kujifungua. Ni nani hasa msichana huyu? Sikiliza makala ya Msichana Jasiri kujua zaidi.
Dora jasiri anaetumia tamthilia kuelimisha juu ya unyanyapaa
Baada ya kutengwa na kunyanyapaliwa na jamii kutokana na maumbile yake, Dora ameamua kutumia filamu kuelimisha jamii kwa njia ya Filamu na tamthilia nchini Tanzania.
Ukurasa uliotangulia
Ukurasa 4 wa 6
Ukurasa unaofuatia