You need to enable JavaScript to run this app.
Nenda kwenye maudhui
Nenda kwenye orodha kuu
Nenda tovuti zaidi za DW
Vidio zetu
Sauti zetu
Maeneo
Tanzania
Kenya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Afrika
Ulaya
Mada
Haki za binadamu
Mazingira
Afya
Teknolojia
Kategoria
Matukio ya Kisiasa
Masuala ya Jamii
Michezo
Yanayoangaziwa
Uchaguzi Mkuu wa Ujerumani 2025
Mzozo wa Israel na Hamas
Bundesliga
Sauti zetu
Vidio zetu
Matangazo
App
Ruka sehemu inayofuata Maudhui yote kwenye mada hii
Maudhui yote kwenye mada hii
Matangazo ya Jioni: 18.01.2025
Stephen Wasira apitishwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania bara. Israel yasema itawaachilia zaidi wafungwa 1900 wa Kipalestina kutoka kwenye magereza yake. Lebanon yasema vikosi vya Israel lazima viondoke nchini mwake kabla ya Januari 26.
Matangazo ya Mchana:18.01.2025
Baraza la mawaziri la Israel laidhinisha makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Israel na Hamas katika Ukanda wa Gaza. Urusi yaushambulia mji mkuu wa Ukraine, watu watatu wauawa. Zaidi ya watu laki mbili wamekimbia ghasia mashariki mwa DRC tangu Januari 1 mwaka huu.
Matangazo ya Asubuhi: 18.01.2025
Taarifa ya Habari ya Asubuhi: 18.01.2025
Baraza la mawaziri la Israel laidhinisha makubaliano ya kusitisha mapigano Gaza na kuachiliwa kwa mateka.+++ Makundi ya kutetea haki za binadamu yanahofia kufanyika kwa "maovu makubwa" huko Uganda wakati nchi hiyo inapojiandaa kwa uchaguzi mkuu mwaka ujao. +++ Umoja wa Mataifa umesema kuwa watu wapatao 230,000 wamekimbia ghasia mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo tangu kuanza kwa 2025.
17.01.2025 Matangazo ya Jioni
Baraza la usalama la Israel limependekeza kukubaliwa kwa mkataba wa usitishaji vita kwenye Ukanda wa Gaza na kuachiliwa kwa mateka wanaoshikiliwa na wanamgambo wa Kipalestina+++Rais wa Iran Masoud Pezeshkian na mwenzake wa Urusi, Vladimir Putin wamesaini ''mkataba wa ushirikano wa kina wa kimkakati'' hatua ambayo huenda ikasababisha wasiwasi kwa serikali za Magharibi.
17.01.2025 Matangazo ya Mchana
Rais Paul Kagame wa Rwanda kwa mara nyingine tena ameilaani jamii ya kimataifa ambayo imekuwa ikikosoa demokrasia nchini Rwanda+++Wapalestina kwenye Ukanda wa Gaza wameanza kurudi kwenye shughuli za maisha ingawa kwa tahadhari wakati wakingojea uamuzi wa baraza la mawaziri la Israel.
Gaza wasubiri kwa hadhari utekelezaji wa usitishaji mapigano
Makubaliano yalifikiwa baada ya miezi 15 za ukanda huo kushambuliwa takribani kila siku na jeshi la Israel.
17.01.2025 Matangazo ya Asubuhi
Ukanda wa Gaza umekumbwa na uharibifu mkubwa kufuatia vita vya zaidi ya miezi 15 kati ya Israel na Hamas+++Nchini Rwanda, malalamiko ya wananchi yanaendelea kufuatia ongezeko la matumizi ya dola za Marekani katika soko la ndani.
17.01.2025 Taarifa ya Habari ya Asubuhi
Marekani imesema ina imani kuwa makubaliano ya kusitisha mapigano huko Gaza yatatekelezwa kama ilivyopangwa. +++ Makumi ya watu wamejeruhiwa na wengine kadhaa wameyakimbia makazi yao kufuatia mapigano mashariki mwa DRC. +++ Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer anatarajiwa kuwasili Poland hivi leo baada ya ziara yake nchini Ukraine.
16.01.2025 Matangazo ya Jioni
Wanamgambo wa Hamas wamepinga madai ya Israel kwamba kundi hilo linajaribu kuzuia makubaliano ya kusitisha mapigano na kurejeshwa kwa mateka yaliyoatangazwa jana Jumatano na wapatanishi wa mzozo baina yao+++Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, CHADEMA leo kinakamilisha hatua yake ya kwanza ya uchaguzi wa mabaraza yake ya uongozi:
16.01.2025 Matangazo ya Mchana
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema Baraza la Mawaziri halitakutana hii leo kuidhinisha makubaliano ya kusitisha mapigano huko Ukanda wa Gaz+++Rais mpya wa Msumbiji ameahidi kuiunganisha nchi yake iliyogawika vibaya kufuatia uchaguzi uliomuweka madarakani.
Chapo aahidi kuiunganisha Msumbiji
Rais mpya wa Msumbiji ameahidi kuiunganisha nchi yake iliyogawika kufuatia uchaguzi uliomuweka madarakani
16.01.2025 Matangazo ya Asubuhi
Rais wa Marekani Joe Biden ametangaza kuwa makubaliano ya usitishaji vita na kuachiliwa kwa mateka yamefikiwa kati ya Israel na Hamas+++Joto la uchaguzi katika chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, CHADEMA, linazidi kushika kasi.
16.01.2025 Taarifa ya Habari ya Asubuhi
Israel na Hamas wafikia makubaliano ya kusitisha mapigano huko Gaza. +++ Waasi wa ADF waua watu 10 mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. +++ Rais wa Marekani Joe Biden atoa hotuba ya kuaga na kuelezea wasiwasi wake kuhusu utawala ujao wa Trump.
15.01.2025 Matangazo ya Jioni
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Shirika la Afya Duniani, WHO limesema mripuko wa ugonjwa unaoshukiwa kuwa ni Marburg umewauwa watu wanane katika vijiji vya mkoa wa Kagera, ulioko kaskazini-magharibi mwa Tanzania/ Makubaliano ya kuvimaliza vita vya Gaza bado yasubiriwa
15.01.2025 Matangazo ya Mchana
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Hamas yakubali rasimu ya makubaliano ya kusitisha vita Gaza/ Urusi yaishambulia Ukraine kwa makombora, droni
Taarifa ya Habari za Ulimwengu Asubuhi Januari 15, 2025
Sikiliza Taarifa ya Habari za Ulimwengu Asubuhi Januari 15, 2025 kutoka Idhaa ya Kiswahili ya DW, Bonn.
14.01.2025 Matangazo ya Jioni
Jumuiya ya Kujihami ya NATO imetangaza kikosi kipya kitakachoilinda miundombinu muhimu ya chini ya bahari katika Bahari ya Baltic+++Takribani watu 100 wameripotiwa kufariki dunia baada ya kukwama kwa miezi kadhaa katika mgodi wa dhahabu uliotelekezwa kaskazini magharibi mwa Afrika Kusini.
14.01.2025 Matangazo ya Mchana
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Makubaliano ya kusitisha vita vya Gaza yanukia/ Waziri wa ulinzi wa Ujerumani aizuru Kiev
14.01.2025 Matangazo ya Asubuhi
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Mazungumzo ya kusitisha vita kati ya Israel na Hamas yapiga hatua kubwa/ Serikali ya mseto ya Kansela Olaf Scholz imeporomoka
13.01.2025 Matangazo ya Jioni
Mwanaharakati na mkosoaji wa serikali ya Tanzania Maria Sarungi amewaambia waandishi wa habari kwamba kamwe hatotishika wala kunyamazishwa// Bunge jipya la Msumbiji limezinduliwa leo Jumatatu sambamba na hafla ya kuwaapisha wabunge wapya// Wazima moto huko Los Angeles nchini Marekani wanaendelea kupambana kuudhibiti moto wa nyika.
Urusi, Iran kusaini mkataba wa ushirikiano wa kimkakati
Urusi imelaumu vikwazo vipya vya Marekani na Uingereza ikisema vinahatarisha biashara ya kimataifa.
Licha ya hali ngumu, Scholz aapa kupambana hadi mwisho
Sabine Kinkartz anasema SPD inategemea siasa za kimataifa zitaibeba kwenye uchaguzi wa Februari 23.
13.01.2025 Matangazo ya Mchana
Jeshi la Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo limesema limeyakomboa maeneo kadhaa wilayani Masisi ambayo yalikuwa yamedhibitiwa na waasi wa M23// Mwanasheria mkuu wa zamani katika serikali ya Rais William Ruto wa Kenya, Justin Muturi amekuwa wa kwanza kuzungumzia wimbi la utekaji nyara vijana wanaoikosoa serikali// Tamasha la ibada linalofahamika kama Kumbh Mela lafunguliwa India.
Ulaya, Arabuni wakutana kuijadili Syria
Mkutano huu unafungua mlango wa ujenzi mpya kwa taifa hilo muhimu kimkakati katika eneo la Mashariki ya Kati.
Taarifa ya Habari za Ulimwengu Asubuhi Januari 13, 2025
Sikiliza Taarifa ya Habari za Ulimwengu Asubuhi Januari 13, 2025 kutoka Idhaa ya Kiswahili ya DW, Bonn.
Matangazo ya Jioni: 12.01.2025
Jeshi la Israel limesema litashambulia kambi ya wakimbizi iliyopo kaskazini mwa Ukanda wa Gaza ya Nuseirat. +++ Umoja wa Ulaya kuamua juu ya kuilegezea vikwazo Syria mwishoni mwa mwezi Januari.+++ Na Urusi yadai kuviteka vijiji viwili mashariki mwa Ukraine.
Matangazo ya Mchana: 12.01.2025
Wanadiplomasia wa nchi za Kiarabu na Ulaya wakutana Saudia kuisaidia Syria.+++ Korea Kusini yathibitisha madai ya Ukraine ya kukamatwa wanajeshi wa Korea Kaskazini huko Kursk.+++ Waliofariki katika moto wa nyika California wafikia 16.
Matagazo ya Jioni 11.01.2025
Ukraine imekuwa ikiwahoji wanajeshi wawili wa Korea Kaskazini+++++Kisiwa cha Mayotte kukabiliwa na kimbunga kipya Jumamosi jioni++++Biden kuongeza muda wa kukaa Marekani kwa wahamiaji wa Venezuela na Sudan++++Ethiopia kufungua soko la hisa ili kuwavutia wawekezaji++++Watu 21 wauawa katika shambulizi la genge nchini Nigeria
Wanajeshi wa Korea Kaskazini wakamatwa na Ukraine
Ukraine imetangaza kuwakamata wanajeshi wawili wa Korea Kaskazini waliokuwa wanapigana upande wa Urusi.
Matangazo ya Dunia Yetu Leo Mchana 11 Januari 2025
Sikiliza Matangazo ya Dunia Yetu Leo Mchana 11 Januari 2025 kutoka Idhaa ya Kiswahili ya DW.
11.01.2025 Taarifa ya Habari ya Asubuhi
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres aitaka Venezuela kuwaachia huru watu wanaoendelea kuzuiliwa bila kufunguliwa mashitaka. Amri ya kutotembea nje yatangazwa Los Angeles, California kufuatia matukio ya moto mkali. Na Marekani na Uingereza zaiwekea vikwazo vipya Urusi.
10.01.2025 Matagazo ya Jioni
Rais wa Venezuela Nicholas Maduro aapishwa kwa muhula wa tatu wa miaka sita+++ Kremlin imesema Rais Vladimir Putin yuko tayari kufanya mazungumzo na Rais mteule wa Marekani, Donald Trump, kuvijadili vita vya Urusi nchini Ukraine +++ UN yasema watoto milioni 3 Sudan wanakabiliwa na utapiamlo mkali +++ Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani kuhudhuria Mkutano wa Syria Saudi Arabia.
10.01.2025 Matangazo ya Mchana
Nchini Tanzania jeshi la polisi limethibitisha kumshikilia Dk. Wibroad Slaa+++Watu wasiopungua 10 wamefariki dunia kwenye moto wa msituni unaoteketeza maeneo ya Los Angeles jimbo la California nchini Marekani+++Rekodi zinaonesha mwaka uliopita wa 2024 ulikuwa mwaka wa kwanza kamili duniani kuwa na ongezeko la joto
10.01.2025 Matangazo ya Asubuhi
Rais wa Venezuela, Nicolás Maduro, anaapishwa hii leo kwa muhula wa tatu+++Joto la kisiasa ndani ya chama kikuu cha upinzani cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA linazidi kupanda huku zikiwa zimebaki siku 10
10.01.2025 Taarifa ya Habari ya Asubuhi
Rais mteule wa Marekani Donald Trump ataka viongozi wa upinzani Venezuela walindwe huku rais Nicholas Maduro akiapishwa leo. Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron azungumza na waziri mkuu wa Uingereza Keir Starmer kuhusu Ukraine na Mashariki ya Kati. Na China yaahidi kulisaidia bara la Afrika na msaada wa kijeshi.
Maduro kuapishwa kwa muhula wa tatu madarakani
Polisi walijitokeza kwa wingi katika mji mkuu Caracas huku upinzani ukiandaa maandamano kupinga kuapishwa Maduro.
09.01.2025 Matangazo ya Jioni
Rais wa Rwanda Paul Kagame ameilaumu jumuiya ya kimataifa ambayo hadi sasa kwa kauli yake imeshindwa kuutatua mzozo wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo+++Bunge nchini Lebanon limepiga kura hivi leo na kumuidhinisha kamanda Jenerali Joseph Aoun kuwa rais mpya wa taifa hilo.
09.01.2025 Matangazo ya Mchana
Nchini Chad watu wenye silaha walivamia makazi ya rais katika mji mkuu wa nchi hiyo, N'Djamena, katika mapigano yaliyosababisha vifo vya watu 19+++Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Msumbiji, aliyekuwa mgombea wa kiti cha urais, Venancio Mondlane amerejea nchini humo.
09.01.2025 Matangazo ya Asubuhi
Bunge la Lebanon linatarajiwa kumchagua rais mpya leo+++Watu 67 wamefariki dunia nchini Rwanda kwa nyakati tofauti kutokana na ugonjwa wa malaria+++Kampuni ya Meta imetangaza kusitisha sera yake ya kuhakiki maudhui yanayochapishwa katika mitandao yake kwa nchini Marekani.
09.01.2025 Taarifa ya Habari ya Asubuhi
Watu 13 wameuwawa katika mji wa Zaporizhzhya kusini mwa Ukraine. Watu 19 wauliwa katika makabiliano makali katika ikulu ya rais nchini Chad. Na Rais wa zamani wa Marekani Jimmy Carter kuzikwa Georgia.
08.01.2025 Matangazo ya Jioni
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken, yuko ziarani nchini Ufaransa kwa mazungumzo kuhusu hali ya Mashariki ya Kati/ Venezuela iko katika harakati za kujiandaa kwa maandamano yanayoiunga mkono na kuipinga serikali kesho Alhamisi
08.01.2025 Matangazo ya Mchana
Miongoni mwa taarifa zilizoandaliwa ni: Rais mteule wa Marekani, Donald Trump, amezuwa mjadala mkali kimataifa baada ya kutaja uwezekano wa kuuchukuwa Mfereji wa Panama, kisiwa cha Greenland na kuigeuza Canada kuwa jimbo la 51 la Marekani/ Kiongozi wa RSF, Mohammed Daglo awekewa vikwazo
Taarifa ya Habari za Ulimwengu Asubuhi 8 Januari 2025
Sikiliza Taarifa ya Habari za Ulimwengu Asubuhi 8 Januari 2025 kutoka Idhaa ya Kiswahili ya DW.
Matangazo ya Dunia Yetu Leo Asubuhi 8 Januari 2025
Sikiliza Matangazo ya Dunia Yetu Leo Asubuhi 8 Januari 2025 kutoka Idhaa ya Kiswahili ya DW.
Trump akosolewa kwa kuashiria kuzitwaa Greenland, Canada
Trump ametowa kauli hiyo chini ya wiki mbili kabla ya kuapishwa rasmi kurejea kwenye Ikulu ya Whitehouse.
Maduro atangaza kukamatwa 'mamluki' wakiwemo Wamarekani
Maduro ametangaza kukamatwa kwa wale aliowaita "mamluki" saba, wakiwemo raia wawili wa Marekani.
Umoja wa Ulaya waituhumu Urusi kwa kutumia gesi kama silaha
Umoja wa Ulaya umeituhumu Urusi kwa kutumia "gesi kama silaha" na kuanzisha vita vya kila upande nchini Moldova.
Jeshi la Uingereza liliuwa kwa makusudi Afghanistan
Wanajeshi wa kikosi maalum cha Uingereza nchini Afghanistan wamesema raia wa Kiafghani wasiokuwa na hatia waliuawa.
RSF imefanya mauaji ya kimbari - Marekani
Marekani imesema kikosi cha RSF kinahusika na mauaji ya kimbari na imetangaza vikwazo dhidi ya kiongozi wa kundi hilo.
Ukurasa uliotangulia
Ukurasa 1 wa 134
Ukurasa unaofuatia